Al-Ahqaf 46:17
الأحقافوَٱلَّذِى قَالَ لِوَٰلِدَيْهِ أُفٍّ لَّكُمَآ أَتَعِدَانِنِىٓ أَنْ أُخْرَجَ وَقَدْ خَلَتِ ٱلْقُرُونُ مِن قَبْلِى وَهُمَا يَسْتَغِيثَانِ ٱللَّهَ وَيْلَكَ ءَامِنْ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ فَيَقُولُ مَا هَـٰذَآ إِلَّآ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
Na yule aliyewafyonya wazazi wake: 'Uff kwenu nyote. Ati ndio mnanitisha kuwa nitafufuliwa, na hali vizazi vingi vimekwisha pita kabla yangu!' Na hao wazazi humwomba msaada Mwenyezi Mungu (na humwambia mtoto wao): 'Ole wako! Amini! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli.' Na yeye husema: 'Hayakuwa haya ila ni visa vya watu wa kale.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ambaye amewafyonya wazazi wake na akawaambia: Ati ndio mnanitisha kuwa nitafufuliwa, na hali vizazi vingi vimekwisha pita kabla yangu! Na hao wazazi humwomba msaada Mwenyezi Mungu (na humwambia mtoto wao): Ole wako! Amini! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Na yeye husema: Hayakuwa haya ila ni visa vya watu wa kale. [17]
[17] Na waliwafyonya wazazi wao kwa kuchukia na kuchoka nao, walipo wataka waamini kufufuliwa, na wakawaambia: Mnaniambia tutatoka makaburini na mataifa mangapi yamepita kabla yangu na hapana hata mmoja aliye fufuliwa kutoka makaburini? Na hao wazazi wake wanaomba msaada kwa Mwenyezi Mungu jinsi ya kuona ni makuu makosa ya mwana wao, wakisema kwa kumshikilia aamini: Utaangamia wewe kama hukuamini. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kufufua ni kweli. Naye bado amekakamia kukadhibisha kwa kusema: Hayo mnayo yasema si chochote ila ni hadithi za uwongo za watu wa kale!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na yule aliyesema kuwaambia wazazi wake wawili walipomlingania kwenye kumuamini Allah Mtukufu na kuamini kuwa kuna kufufuliwa, “Ubaya wenu! Je mnaniahidi kuwa nitatolewa kaburini mwangu nikiwa hai na hali kwamba makarne ya ummah kabla yangu yashapita, na hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyefufuliwa?” Na hali wazazi wake wanamuomba Allah Mtukufu Amuongoze na huku wakimwambia, “Ole wako! Amini na usadiki na ufanye matendo mema, hakika ahadi ya Allah Mtukufu ni kweli isiyokuwa na shaka.” Hapo awaambie, Hayakuwa haya mnayoyasema isipokuwa ni mambo ya urongo waliyoyaandika watu wa mwanzo, yamenukuliwa kwenye vitabu vyao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net