Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 16

Al-Ahqaf 46:16

الأحقاف

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ نَتَقَبَّلُ عَنْهُمْ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا۟ وَنَتَجَاوَزُ عَن سَيِّـَٔاتِهِمْ فِىٓ أَصْحَـٰبِ ٱلْجَنَّةِ ۖ وَعْدَ ٱلصِّدْقِ ٱلَّذِى كَانُوا۟ يُوعَدُونَ

Maana

Hao ndio tunaowapokelea bora ya vitendo vyao walivyovitenda, na tunayasamehe makosa yao. Watakuwa miongoni mwa watu wa Bustani za mbinguni. Miadi ya kweli hiyo waliyokuwa wakiahidiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio tunao wapokelea bora ya vitendo vyao walivyo vitenda, na tunayasamehe makosa yao. Watakuwa miongoni mwa watu wa Peponi. Miadi ya kweli hiyo walio ahidiwa. [16]

[16] Hao walio sifika kwa sifa hizo ndio tutakao wapokelea a'mali zao njema, na tutawasamehe maovu yao miongoni mwa watu wa Peponi. Itawathibitikia miadi ya kweli walio kuwa wakiahidiwa duniani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio ambao tutayapokea kutoka kwao mazuri zaidi ya matendo mema waliyoyafanya, na tutasamehe dhambi zao, wakiwa ni miongoni mwa watu wa Peponi. Ahadi hii tuliyowaahidi ni ahadi ya ukweli na haki isiyokuwa na shaka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net