Al-Jaathiya 45:9
الجاثيةوَإِذَا عَلِمَ مِنْ ءَايَـٰتِنَا شَيْـًٔا ٱتَّخَذَهَا هُزُوًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ
Na anapokijua kitu kidogo katika Aya zetu, hukifanyia mzaha. Watu hao ndio watakaokuwa na adhabu ya kufedhehesha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na anapo kijua kitu kidogo katika Aya zetu hukifanyia mzaha. Watu hao ndio watakao kuwa na adhabu ya kufedhehesha. [9]
[9] Na huyu mwenye inda, akijua kitu kidogo katika Aya za Mwenyezi Mungu huzifanya Aya zote za Mwenyezi Mungu ni kitu cha kufanyia maskhara na mzaha. Wazushi hao wingi wa madhambi watapata adhabu ya kuwadhalilisha kwa kiburi chao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na huyu mrongo mwingi wa dhambi anapojua kitu katika aya zetu anazifanyia shere na mzaha. Hao watakuwa na adhabu itakayowadhalilisha na kuwatia kwenye hizaya Siku ya Kiyama, ikiwa ni malipo ya kuicheza shere kwao Qur’ani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net