Al-Jaathiya 45:8
الجاثيةيَسْمَعُ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Anayesikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anashikilia yale yale aliyokatazwa, na anajivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Anaye sikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anashikilia yale yale aliyo katazwa, na anajivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu! [8]
[8] Mzushi kama huyu husikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, nazo zinasema haki tupu. Kisha yeye huendelea na ukafiri wake kwa kutakabari, akaikataa Imani. Hali yake ni hali ya asiye pata kuzisikia Aya. Basi ewe Nabii! Mbashirie, kwa kumkejeli, kuwa atapata adhabu chungu kwa huko kushikilia kwake kitendo kitacho mletea adhabu hiyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Anayezisikia aya za kitabu cha Allah Mtukufu akisomewa kisha akaendelea kwenye ukanushaji wake kwa kujiona ni mkubwa zaidi wa kutoweza kumfuata Allah Mtukufu na Mtume wake, kana kwamba hakusikia alichosomewa miongoni mwa aya za Allah Mtukufu. Basi mbashirie, ewe Mtume, huyo mrongo mwenye dhambi nyingi: adhabu yenye uchungu inayoumiza ndani ya Moto wa Jahanamu Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net