Al-Jaathiya 45:10
الجاثيةمِّن وَرَآئِهِمْ جَهَنَّمُ ۖ وَلَا يُغْنِى عَنْهُم مَّا كَسَبُوا۟ شَيْـًٔا وَلَا مَا ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوْلِيَآءَ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Na nyuma yao ipo Jahanamu. Na waliyoyachuma hayatawafaa hata kidogo, wala walinzi waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu. Na watapata adhabu kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nyuma yao ipo Jahannamu. Na walio yachuma hayatawafaa hata kidogo, wala walinzi walio washika badala ya Mwenyezi Mungu. Na watapata adhabu kubwa. [10]
[10] Nyuma yao ipo Jahannamu inawangojea, na walicho kichuma duniani hakitawapunguzia hata chembe ya adhabu yake. Wala hiyo miungu ya uwongo walio ifanya ndio ya kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu, haitawakinga na chochote katika adhabu yake. Na wao watapata mateso makubwa, kwa kitisho chake na ukali wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi mbele ya hao wenye kuzifanyia shere aya za Allah Mtukufu patakuwa na moto wa Jahanamu. Na hakitawafaa kitu chochote walichokichuma cha mali na watoto wala waungu wao waliowaabudu badala ya Allah Mtukufu. Na watakuwa na adhabu kubwa yenye uchungu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net