Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 5

Al-Jaathiya 45:5

الجاثية

وَٱخْتِلَـٰفِ ٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ وَمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن رِّزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ ٱلْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَتَصْرِيفِ ٱلرِّيَـٰحِ ءَايَـٰتٌ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

Maana

Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayoiteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili. [5]

[5] Na katika kukhitalifiana usiku na mchana, kwa urefu na ufupi, na mwangaza na giza, na kupeana zamu kwa nidhamu iliyo thibiti, na katika mvua anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, akaihuisha ardhi kwa mimea baada ya kufa kwake kwa ukame, na kuziendesha pepo pande mbali mbali nazo zinakhitalifiana kwa ubaridi na joto, na nguvu na udhaifu, ni alama zilizo wazi za kuonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye kufikiri kwa akili zao, wakafikilia yakini yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na katika kupishana usiku na mchana na kufuatana, na katika kuwaletea mvua anayoiteremsha Allah Mtukufu kutoka mawinguni, Akaihuisha kwayo ardhi baada ukavu wake, ikasheheni mimea na mazao, na katika kuwaletea upepo kutoka sehemu zote, na kuufanya uwe kwa maslahi yenu, kuna dalili na hoja kwa watu wanaoelewa kuhusu Allah Mtukufu, hoja Zake na dalili Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net