Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 6

Al-Jaathiya 45:6

الجاثية

تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱللَّهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِٱلْحَقِّ ۖ فَبِأَىِّ حَدِيثٍۭ بَعْدَ ٱللَّهِ وَءَايَـٰتِهِۦ يُؤْمِنُونَ

Maana

Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayoiamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayo iamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake? [6]

[6] Hizo ni Aya za Mwenyezi Mungu zinazo eleza uumbaji alio ufanya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya watu. Tunakusomea wewe katika Qur'ani kwa ulimi wa Jibrili, nazo Aya hizo ni za haki. Ikiwa hao hawaziamini hizi basi maneno gani watayasadiki baada ya maneno ya Mwenyezi Mungu, nayo ni Qur'ani na Aya zake

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Aya hizi na hoja hizi tunakusomea wewe, Mtume, kwa haki. Basi ni mazungumzo gani baada ya Allah Mtukufu na dalili Zake kuwa Yeye Ndiye Mola wa kweli Peke Yake, Hana mshirika, watayaamini na kuyakubali na kuyatumia?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net