Al-Jaathiya 45:4
الجاثيةوَفِى خَلْقِكُمْ وَمَا يَبُثُّ مِن دَآبَّةٍ ءَايَـٰتٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ
Na katika umbo lenu na katika wanyama aliowatawanya, zimo Ishara kwa watu wenye yakini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika umbo lenu na katika wanyama alio watawanya zimo Ishara kwa watu wenye yakini. [4]
[4] Na vile Mwenyezi Mungu kukuumbeni nyinyi, enyi watu, kama mlivyo, mna sura nzuri, na umbo la peke yenu, na mnavyo khitalifiana baina ya wanaadamu na wanyama na mkaenezwa ulimwenguni, na manufaa mbali mbali, bila ya shaka ni Ishara zenye nguvu na ziwazi kwa watu wanao tafuta yakini ya mambo yao kwa kuzingatia na kufikiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na katika kuwaumba nyinyi, enyi watu, na uumbaji wa vilivyotapakaa ardhini miongoni mwa vinavyotambaa juu yake, kuna hoja na dalili kwa watu wenye imani ya yakini juu ya Allah Mtukufu na Sheria Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net