Al-Jaathiya 45:3
الجاثيةإِنَّ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ لَـَٔايَـٰتٍ لِّلْمُؤْمِنِينَ
Hakika katika mbingu na ardhi ziko Ishara kwa Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika katika mbingu na ardhi ziko Ishara kwa Waumini. [3]
[3] Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi ni katika ufundi wa namna ya pekee wa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka ni dalili zenye nguvu kabisa katika Ungu wake na Upweke wake, ambao wanauamini wenye kumsadiki Mwenyezi Mungu kwa maumbile yao yaliyo sawa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika kwenye mbingu saba na ardhi ambapo humo viumbe vinatoka, na vilivyomo baina ya hivyo viwili miongoni mwa viumbe wa jinsi tofauti na aina mbalimbali, kuna dalili na hoja kwa wenye kuziamini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net