Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 36

Al-Jaathiya 45:36

الجاثية

فَلِلَّهِ ٱلْحَمْدُ رَبِّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَرَبِّ ٱلْأَرْضِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu, na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote. [36]

[36] Basi ni za Mwenyezi Mungu pekee sifa njema, Muumba mbingu na ardhi, na Muumba wa viumbe vyote. Kwani hivi kuwa ni Mola Mlezi wa kila kitu unawajibika uhimidiwe kwa neema zote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi ni za Allah Mtukufu, kutakasika ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Peke Yake, shukrani zote kwa neema Zake zisizohesabika kwa viumbe Vyake, Mola wa mbingu na ardhi na Mwenye kuziumba na kuziendesha, Mola wa viumbe Wote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net