Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 35

Al-Jaathiya 45:35

الجاثية

ذَٰلِكُم بِأَنَّكُمُ ٱتَّخَذْتُمْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ هُزُوًا وَغَرَّتْكُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا ۚ فَٱلْيَوْمَ لَا يُخْرَجُونَ مِنْهَا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ

Maana

Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu; na maisha ya dunia yakakudanganyeni. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao. [35]

[35] Adhabu hiyo imekuteremkieni kwa sababu ya ukafiri wenu, na maskhara yenu kuzifanyia Ishara za Mwenyezi Mungu, na mlivyo khadaika na maisha ya dunia kwa mapambo yake. Basi leo hapana yeyote awezaye kuwatoa hawa kwenye Moto, wala hawatakikani kumtaka radhi Mola wao Mlezi kwa kutafuta udhuru.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Haya yaliyowafika ya adhabu ya Allah Mtukufu ni kwa sababu ya kuwa nyinyi mlizifanya aya za Allah Mtukufu na hoja Zake kuwa shere na mchezo, na likawadanganya pambo la uhai wa kilimwengu. Basi Leo hawatatolewa Motoni wala hawatarudishwa ulimwenguni ili watubie na wafanye mema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net