Al-Jaathiya 45:34
الجاثيةوَقِيلَ ٱلْيَوْمَ نَنسَىٰكُمْ كَمَا نَسِيتُمْ لِقَآءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا وَمَأْوَىٰكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّـٰصِرِينَ
Na itasemwa: 'Leo tunawasahau kama nyinyi mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wowote wa kuwanusuru.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na itasemwa: Leo tunakusahauni kama nyinyi mlivyo sahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wa kukunusuruni. [34]
[34] Na wataambiwa hawa washirikina kwa kuwahizi: Leo hii tunakuacheni katika adhabu kama nyinyi mlivyo acha kujitayarisha kukutana na Mola wenu Mlezi katika siku hii kwa ut'iifu na vitendo vyema. Na pahala penu pa kukaa ni Motoni, na wala hamna wa kukunusuruni akakuokoeni na adhabu yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wakaambiwa hao makafiri, Leo tutawaacha ndani ya adhabu ya Moto wa Jahanamu, kama vile mlivyoacha kumuamini Mola wenu na kufanya matendo ya kuwafaa katika makutano ya Siku yenu hii, na makao yenu ni Moto wa Jahanamu, na hamtakuwa na wasaidizi wenye kuwaokoa na adhabu ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net