Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 33

Al-Jaathiya 45:33

الجاثية

وَبَدَا لَهُمْ سَيِّـَٔاتُ مَا عَمِلُوا۟ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Maana

Basi ubaya wa yale waliyoyatenda utawadhihirikia, na yatawafika yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi ubaya wa waliyo yatenda utawadhihirikia, na yatawazunguka waliyo yafanyia maskhara. [33]

[33] Na utawadhihirikia hawa makafiri ubaya wa vitendo vyao, na itawateremkia jaza ya maskhara yao waliyo kuwa wakizifanyia Ishara za Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yakawadhihirikia hawa waliokuwa wakizikanusha aya za Allah Mtukufu yale matendo mabaya waliyoyafanya ulimwenguni, na ikawateremkia adhabu ya Allah Mtukufu ikiwa ni malipo ya yale waliokuwa wakiyafanyia shere.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net