Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 32

Al-Jaathiya 45:32

الجاثية

وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ وَٱلسَّاعَةُ لَا رَيْبَ فِيهَا قُلْتُم مَّا نَدْرِى مَا ٱلسَّاعَةُ إِن نَّظُنُّ إِلَّا ظَنًّا وَمَا نَحْنُ بِمُسْتَيْقِنِينَ

Maana

Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Saa haina shaka, nyinyi mlikuwa mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, na Saa haina shaka, nyinyi mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini. [32]

[32] Enyi mnao kanya kufufuliwa! Akikwambieni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba agano la Mwenyezi Mungu la kuwalipa ni haki yenye kuthibiti, na Saa haina shaka itakuja, nyinyi mkisema: Sisi hatujui chochote khabari ya hiyo Saa ya Kiyama, wala ukweli wake; na sisi ni dhana ya kudhania tu kuwa hiyo Saa itakuja, wala hatuna yakini kuwa itatokea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mnapoambiwa, «Hakika ahadi ya Allah Mtukufu ya kuwafufua watu kutoka kwenye makaburi yao ni kweli, na kwamba kipindi cha kusimama Kiyama ni jambo lisilo na shaka, mnasema, “Hatujui ni nini Kiyama? Na hatuamini kuwa kitatokea isipokuwa ni kudhania tu, na sisi si wenye uhakika kuwa kipindi hicho cha Kiyama ni chenye kuja”».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net