Al-Jaathiya 45:37
الجاثيةوَلَهُ ٱلْكِبْرِيَآءُ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ
Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [37]
[37] Na ni wake Yeye, Subhanahu, utukufu na utawala katika mbingu na ardhi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, asiye shindika, Mwenye hikima, asiye kosea katika hikima yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ni wake Peke Yake utukufu, haiba, utawala, uwezo na ukamilifu, mbinguni na ardhini. Na Yeye Ndiye Mshindi Asiyekuwa na mshindani mwenye kushindana na Yeye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake, vitendo Vyake, upangaji Wake na Sheria Zake, Ametukuka na kutakasika, hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net