Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 26

Al-Jaathiya 45:26

الجاثية

قُلِ ٱللَّهُ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يَجْمَعُكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Maana

Sema: 'Mwenyezi Mungu anawahuisha, kisha anawafisha, kisha atawakusanya Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mwenyezi Mungu anakuhuisheni, kisha anakufisheni, kisha anakukusanyeni Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui. [26]

[26] Ewe Muhammad! Waambie: Mwenyezi Mungu amekupeni uhai duniani nanyi hamkuwa chochote, kisha anakufisheni unapo timia wakati wenu. Kisha atakukusanyeni Siku ya Kiyama, na hapana shaka ya kukusanywa huko. Lakini wengi wa watu hawaujui uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kufufua, kwa sababu ya mapuuza yao kuzingatia dalili ziliopo. Na huyo Muweza wa hayo pia ni Muweza wa kuwaleta baba zenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina wenye kukanusha kufufuliwa, “Allah Mtukufu Aliyetakasika na kutukuka, Atawahuisha duniani kipindi Anachotaka muishi, kisha Atawafisha humo, kisha Atawakusanya mkiwa hai kwenye Siku ya Kiyama isiyokuwa na shaka. Lakini wengi wa watu hawajui kwamba Allah Mtukufu ni Muweza wa kuwafisha, kisha kuwafufua Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net