Al-Jaathiya 45:25
الجاثيةوَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتُنَا بَيِّنَـٰتٍ مَّا كَانَ حُجَّتَهُمْ إِلَّآ أَن قَالُوا۟ ٱئْتُوا۟ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: 'Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wasemao kweli.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wasemao kweli. [25]
[25] Na ukiwasomea Aya za Mwenyezi Mungu zilizo wazi zenye kuonyesha uwezo wake wa kufufua, huwa hawana hoja ila kusema - kwa kuikimbia haki : Wafufueni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wasema kweli katika kudai kuwa kupo kufufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanaposomewa, hawa washirikina wakanushaji, aya zetu zilizo wazi, huwa hawana hoja isipokuwa ni kutoa maneno yao kumwambia Mtume Muhammad, “Wahuishe, wewe na Waumini, baba zetu waliokufa iwapo nyinyi ni wakweli kwa mnayoyasema”.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net