Al-Jaathiya 45:27
الجاثيةوَلِلَّهِ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَيَوْمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَخْسَرُ ٱلْمُبْطِلُونَ
Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, siku hiyo wataangamia wenye kushikamana na upotovu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na siku itapo simama Saa ya Kiyama, siku hiyo wataangamia wenye kushikamana na upotovu. [27]
[27] Na ni wa Mwenyezi Mungu pekee ufalme wa mbingu na ardhi, kwa kuumba, kumiliki, na kupanga. Na itapo fika Saa ya Kiyama, siku hiyo watakhasiri wenye kufuata upotovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni ya Allah Mtukufu, Aliyetakasika, mamlaka ya mbingu saba na ardhi kwa kuziumba, kuzimiliki na kuwa ziko chini ya amri Yake. Na siku Kiyama kitakapokuja ambapo wafu watafufuliwa kutoka kwenye makaburi yao na watahesabiwa, hapo watapata hasara wale waliomkanusha Allah Mtukufu na kukataa kile Alichomteremshia Mtume Wake miongoni mwa aya zilizobainika na dalili zilizodhihiri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net