Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 21

Al-Jaathiya 45:21

الجاثية

أَمْ حَسِبَ ٱلَّذِينَ ٱجْتَرَحُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن نَّجْعَلَهُمْ كَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ سَوَآءً مَّحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ ۚ سَآءَ مَا يَحْكُمُونَ

Maana

Je, wanadhani wale wanaotenda maovu kuwa tutawafanya wawe sawasawa na wale walioamini, na wakatenda mema, uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya mno wanayoihukumu!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Wanadhani wanao tenda maovu kuwa tutawafanya kama walio amini, na wakatenda mema, sawa sawa uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya wanayo ihukumu! [21]

[21] Bali wanadhani hao walio chuma yanayo chusha katika ukafiri na maasi kwamba tutawafanya kama walio muamini Mwenyezi Mungu na wakatenda vitendo vyema, na hivyo tuwafanye sawa baina ya makundi mawili hayo katika uhai na katika kufa? Hukumu yao ni mbaya mno, ikiwa wanahisi kuwa wao ni sawa na Waumini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hivi wanadhani wale wanaotenda maovu na wanaowakanusha Mitume wa Allah Mtukufu na kuenda kinyume na amri ya Mola wao na wakamuabudu asiyekuwa Yeye, kuwa tutawafanya ni kama wale wanaomuamini Allah Mtukufu na wakawaamini Mitume Wake na wakafanya matendo mema na wakamtakasia Yeye ibada na sio wengine? wanadhani tutawafanya wawe sawa ulimwenguni na Akhera? Ni uamuzi mbaya huo wao wa kulinganisha baina ya waovu na wema kesho Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net