Al-Jaathiya 45:20
الجاثيةهَـٰذَا بَصَـٰٓئِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ
Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uongofu na rehema kwa watu wenye yakini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu, na rehema kwa watu wanao yakinisha. [20]
[20] Hii Qur'ani ulio teremshiwa wewe ni dalili kwa watu kuwaonyesha Dini ya Haki, na uwongofu wa kuwaongoza kwenye njia za kheri, na neema kwa watu wenye kuyakinisha thawabu na adhabu za Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hii Qur’ani tuliyokuteremshia, ewe Mtume, ni muangaza wa watu kuiona haki na kuipambanua na batili, na kuijua kwayo njia ya usawa, na ni uongofu na rehema kwa watu wenye kuwa na Imani ya yakini juu ya uhakika wa usahihi wake, na kwamba hiyo ni teremsho kutoka kwa Mshindi Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net