Al-Jaathiya 45:19
الجاثيةإِنَّهُمْ لَن يُغْنُوا۟ عَنكَ مِنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا ۚ وَإِنَّ ٱلظَّـٰلِمِينَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ ۖ وَٱللَّهُ وَلِىُّ ٱلْمُتَّقِينَ
Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki msaidizi wa wamchao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki wa wamchao. [19]
[19] Hakika hao waongo wenye tamaa ya kuwa ati wewe utawafuata wao, hawatoweza kukuondolea hata chembe ya adhabu pindi ukiwafuata. Na hakika wenye kupindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu husaidiana wao kwa wao katika upotovu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuwasaidia wale wanao mcha, basi hao haitawafikia dhulma ya wenye kudhulumu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa waliomshirikisha Mola wao wanaokuita ufuate matamanio yao, hawatakufaa kitu, ewe Mtume, kwa kukuepushia adhabu ya Allah Mtukufu iwapo utafuata matamanio yao. Na hakika madhalimu wenye kukiuka mipaka ya Allah Mtukufu miongoni mwa wanafiki, Mayahudi na wasiokuwa hao wanasaidiana wao kwa wao dhidi ya wenye kumuamini Allah Mtukufu na walio watiifu Kwake. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuwapa ushindi wenye kumcha Mola wao kwa kutekeleza faradhi Zake na kujiepusha na makatazo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net