Al-Jaathiya 45:18
الجاثيةثُمَّ جَعَلْنَـٰكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ ٱلْأَمْرِ فَٱتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَآءَ ٱلَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ
Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasiojua kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu. [18]
[18] Tena tukakujaalia wewe, ewe Muhammad, baada ya khitilafu za Watu wa Kitabu (yaani Mayahudi na Wakristo), kuwa ni Mtume wa kwenda Njia iliyo wazi katika mambo ya Dini tuliyo kuwekea wewe na walio kuwa kabla yako miongoni mwa Mitume. Basi ifuate Sharia yako ya Haki, yenye kuthibiti imara kwa hoja na dalili, wala usifuate matamanio ya watu wasio ijua Njia ya Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha tukakufanya, ewe Mtume, uwe kwenye njia iliyo wazi kuhusu jambo la Dini. Basi fuata Sheria ambayo Allah Mtukufu Amekupatia, na usifuate matamanio ya wajinga wasiojua Sheria ya Allah Mtukufu, wasiojua haki. Katika hii aya kuna ushahidi mkubwa juu ya ukamilifu wa Dini hii na utukufu wake, na ulazima wa kufuata hukumu zake na kutopotoka kuelemea kwenye matamanio ya makafiri na wapotofu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net