Al-Jaathiya 45:17
الجاثيةوَءَاتَيْنَـٰهُم بَيِّنَـٰتٍ مِّنَ ٱلْأَمْرِ ۖ فَمَا ٱخْتَلَفُوٓا۟ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلْعِلْمُ بَغْيًۢا بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِى بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ فِيمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Na tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakuhitalifiana ila baada ya kuwajia elimu kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyokuwa wakihitilafiana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa ajili ya uhasidi uliyo kuwa baina yao. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyo kuwa wakikhitalifiana. [17]
[17] Na tumewapa dalili wazi katika mambo ya Dini yao. Basi haikutokea khitilafu baina yao ila baada ya kwisha wajia ujuzi wa hakika ya Dini na hukumu zake. Na hayo ni kwa uadui na uhasidi tu ulio baina yao. Hakika Mola wako Mlezi atapambanua baina ya hao wanao khitalifiana Siku ya Kiyama katika mambo waliyo kuwa wamekhitalifiana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukawapatia Wana wa Isrãîl Sheria zilizo wazi juu ya halali na haramu, na dalili zenye kutenganisha haki na batili. Hawakutafautiana isipokuwa baada ya kujiwa na elimu na hoja ikasimama juu yao. Na lililowapelekea wafanye hivyo ni lile jambo la kudhulumiana wao kwa wao kwa kutaka ukubwa na uongozi. Hakika Mola wako Atahukumu baina ya wanaotafautiana miongoni mwa Wana wa Isrãîl Siku ya Kiyama katika yale waliokuwa wakitafautiana juu yake duniani. Kwenye maelezo haya pana onyo kwa ummah huu wasifuate mwenendo wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net