Al-Jaathiya 45:16
الجاثيةوَلَقَدْ ءَاتَيْنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحُكْمَ وَٱلنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَـٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ وَفَضَّلْنَـٰهُمْ عَلَى ٱلْعَـٰلَمِينَ
Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu, hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote. [16]
[16] Ninaapa kwa hakika tumewapa Wana wa Israili Taurati, na hukumu iliomo ndani yake, na Unabii ulio funuliwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na tumewaruzuku kheri namna mbali mbali, na tumewafadhilisha wao katika neema nyingi juu ya viumbe vyote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika tuliwapatia Wana wa Isrãîl Taurati na Injili, na tukawaamuru kuhukumu kulingana na yaliyomo kwenye vitabu viwili hivyo, na tukawafanya wengi wa Manabii watokanao na kizazi cha Ibrãhîm, amani imshukie, ni katika wao, na tukawaruzuku vitu vizuri miongoni mwa vitu vya kukimu maisha, matunda na vyakula, na tukawafadhilisha juu ya walimwengu wa zama zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net