Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 15

Al-Jaathiya 45:15

الجاثية

مَنْ عَمِلَ صَـٰلِحًا فَلِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَنْ أَسَآءَ فَعَلَيْهَا ۖ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ

Maana

Mwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda uovu ni juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda uovu ni juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi. [15]

[15] Mwenye kutenda mema atapata ujira wake na thawabu mwenyewe; na mwenye kutenda uovu basi dhambi za kitendo chake zitamuangukia mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Muumba wenu kwa ajili ya malipo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yoyote, miongoni mwa waja wa Allah Mtukufu, Anayefanya matendo ya utiifu Kwake, basi malipo mema ya utiifu wake atayapata mwenyewe, na mwenye kufanya matendo mabaya duniani kwa kumuasi Allah Mtukufu, basi atakuwa amejikosea mwenyewe. Kisha nyinyi, enyi watu, mtaishia kwa Mola wenu baada ya kufa kwenu, Amlipe mwema kwa wema wake na mbaya kwa ubaya wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net