Al-Jaathiya 45:14
الجاثيةقُل لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يَغْفِرُوا۟ لِلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ أَيَّامَ ٱللَّهِ لِيَجْزِىَ قَوْمًۢا بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
Waambie walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyokuwa wakiyachuma.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Waambie walio amini wawasamehe wale wasio zitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyo kuwa wakiyachuma. [14]
[14] Ewe Mtume! Waambie wanao msadiki Mwenyezi Mungu na wanakufuata wewe, wasamehe maudhi yanayo wafikia kutokana na watu ambao hawataraji kuja siku za Mwenyezi Mungu za kuwalipa watu kwa kheri na shari kwa mujibu walivyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, uwaambie wenye kumuamini Allah Mtukufu na wakamfuata Mtume Wake, wawasamehe na kuwaachia wale ambao hawana matarajio ya malipo mema ya Allah Mtukufu, na hawaogopi adhabu Yake, pindi wanapowakusudia kwa ajili ya Waumini kuwaudhi na kuwakera, ili Allah Mtukufu Awalipe washirikina hawa kwa yale waliyoyachuma duniani ya madhambi na kuwaudhi Waumini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net