Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 13

Al-Jaathiya 45:13

الجاثية

وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا مِّنْهُ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Maana

Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri. [13]

[13] Na akakudhalilishieni vyote viliomo mbinguni, nyota zenye kung'ara na sayari, na vyote viliomo kwenye ardhi, makulima, mifugo, maji, moto, hewa, na jangwa, vyote hivyo vinatokana na Yeye Mtukufu, ili akuenezeeni manufaa ya uhai. Hakika katika hizo neema zilizo tajwa zipo Ishara zenye kuonyesha kudra yake kwa watu wenye kuzingatia Ishara.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Akawadhalilishia kila kilichoko mbinguni miongoni mwa jua, mwezi na nyota, na kila kilicho ardhini miongoni mwa wanyama, miti, majahazi na visivyokuwa hivyo kwa ajili ya maslahi yenu. Neema zote hizi ni vipaji alivyowaneemesha navyo Allah Mtukufu Peke Yake na fadhila inayotoka Kwake Aliyowafadhili nayo. Basi Yeye Peke Yake muabuduni, na msimfanye yoyote kuwa ni mshirika Wake. Hakika katika vitu Alivyowadhalilishia Allah Mtukufu kuna alama na dalili juu ya upweke wa Allah Mtukufu kwa watu wenye kuzitia akilini aya za Allah Mtukufu, hoja Zake na dalili Zake, wakazizingatia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net