Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 36

Ad-Dukhaan 44:36

الدخان

فَأْتُوا۟ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ

Maana

Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. [36]

[36] Na wao humwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini: Ikiwa nyinyi mnasema kweli katika madai yenu kwamba Mola wenu Mlezi anahuisha wafu kwa ajili ya hisabu katika Akhera, basi upesi upesi tufufulieni baba zetu walio kwisha kufa, kwa kumwomba huyo Mola wenu Mlezi!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wanasema pia, «Basi tuletee, ewe Muhammad: wewe na walio pamoja na wewe, wazazi wetu waliokufa, iwapo nyinyi ni wakweli kwamba Allah Mtukufu Atawafufua walio makaburini wakiwa hai».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net