Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 37

Ad-Dukhaan 44:37

الدخان

أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ أَهْلَكْنَـٰهُمْ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ مُجْرِمِينَ

Maana

Je, ni wao bora au watu wa Tubbaa' na waliokuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu. [37]

[37] Je! Makafiri wa Makka wanawashinda kaumu ya Tubbaa' na walio watangulia kwa nguvu, na ulinzi, na utawala, na mambo yote ya kidunia? Ewe Muhammad! Hao washirikina wa kaumu yako hawawashindi hao kwa nguvu, na hao Sisi tuliwateketeza katika dunia kwa ukafiri wao na madhambi yao. Basi nawawazingatie!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, hawa washirikina ni bora au watu wa Tubba’ (wa Himyar) na wale waliokuwa kabla yao miongoni mwa ummah waliomkanusha Mola wao? Tuliwaangamiza kwa uhalifu wao na kukanusha kwao. Hawa washirikina si bora kuliko hao mpaka eti tuwasamehe na tusiwaangamize, na hali wao wanamkanusha Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net