Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 35

Ad-Dukhaan 44:35

الدخان

إِنْ هِىَ إِلَّا مَوْتَتُنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ

Maana

Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi. [35]

[35] Hakika hawa wanao kadhibisha kufufuliwa bila ya shaka wanasema: Hapana kufa ila kwa haya haya mauti yetu ya kwanza ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa tena.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakuna kifo chochote ila kile kifo chetu tutakachokufia, nacho ndicho kifo cha mwanzo na cha mwisho, na sisi baada ya kufa kwetu hatutakuwa ni wenye kufufuliwa tuhesabiwe na tulipwe mema au tuteswe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net