Ad-Dukhaan 44:24
الدخانوَٱتْرُكِ ٱلْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ
Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao ni jeshi litakalozamishwa.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa. [24]
[24] Na iache bahari imetulia kama ilivyo baada ya kwisha pigwa kwa fimbo, wapate kuingia hao wanao kanya; kwani wao watazama tu, hapana hivi wala hivi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na iache bahari kama ilivyo utakapopita, ikiwa imetulia haina mchafuko. Hakika Fir’awn na askari wake ni wenye kuzamishwa humo baharini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net