Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 23

Ad-Dukhaan 44:23

الدخان

فَأَسْرِ بِعِبَادِى لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ

Maana

Mwenyezi Mungu akasema: 'Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa. [23]

[23] (Naye Musa akaambiwa:) Toka na Waumini usiku usiku kwa kificho, wasije kukupateni, kwani Firauni na askari wake watakufuateni pindi wakijua, wakukamateni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi nenda na waja wangu waliokuamini, wakakukubali na wakakufuata, ewe Mûsã, katika kipindi cha usiku, kwani nyinyi mtafuatwa na Fir’awn na askari wake. Na nyinyi mtaokolewa, na Fir’awn na askari wake watazama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net