Ad-Dukhaan 44:25
الدخانكَمْ تَرَكُوا۟ مِن جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ
Mabustani mangapi na chemchemi ngapi waliziacha!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha! [25]
[25] Hao watu wa Firauni baada ya kuzama kwao waliacha mabustani mengi yenye kunawiri, na chemchem zinazo tiririka maji yake,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni vingapi alivyoviacha Fir’awn na watu wake, baada ya kuangamia kwao na kuzamishwa baharini na Allah Mtukufu, miongoni mwa mabustani na mashamba yaliyostawi, chemchemi za maji yenye kupita?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net