Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 80

Az-Zukhruf 43:80

الزخرف

أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَىٰهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ

Maana

Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong'ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong'ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika. [80]

[80] Ati wanadhani hawa washirikina kwamba Sisi hatuyasikii maneno yao wenyewe wanapo panga njama, na wanapo semezana kwa siri katika kukanusha haki? Kwani! Twawasikia. Na Malaika wanao dhibiti kauli zao wanayaandika hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au kwani wanadhani, hawa wenye kumshirikisha Allah Mtukufu, kuwa sisi hatusikii yale wanayoyaficha ndani ya nafsi zao na kunong’onezana baina yao? Basi sivyo hivyo, sisi tunasikia na tunajua, na wajumbe wetu ambao ni Malaika watukufu wanawaandikia yote waliyoyafanya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net