Az-Zukhruf 43:79
الزخرفأَمْ أَبْرَمُوٓا۟ أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ
Au waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunaopitisha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunao pitisha. [79]
[79] Kwani ndio waliweza washirikina wa Makka kutimiza hivyo vituko vyao kumkadhibisha Mtume na kupanga njama za kumuuwa? Bali Sisi kwa hakika tuliweza jambo katika kuwalipizia wao na kukupa ushindi wewe juu yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hivi hawa washirikina wamepanga mambo madhubuti ya kuipinga haki tuliyowaletea? Sisi tunawapangia adhabu na mateso.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net