Az-Zukhruf 43:81
الزخرفقُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلْعَـٰبِدِينَ
Sema: 'Ingelikuwa Rahmani (Mwingi wa Rehema) ana mwana, basi mimi ningelikuwa wa kwanza kumuabudu.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Ingeli kuwa Rahmani ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu. [81]
[81] Waambie hao washirikina: Ikithibitika kwa ushahidi kuwa kweli Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu mwana huyo. Lakini hayo hayakuthibiti kwa hoja yoyote kwamba Rahmani ana mwana, kwa kuwa hayo ni kumfanya Mwenye nguvu awe hajiwezi, Mwenye kujitosha awe mhitaji. Na Yeye, Subhanahu, ametakasika na kila la upungufu kwa ukamilifu wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe mtume, uwaambie washirikina wa watu wako wanaodai kuwa Malaika ni watoto wa kike wa Allah Mtukufu, «Ingekua Mwingi wa rehema ana mtoto, kama mnavyodai, -lakini hili halikuwa wala halitakuwa-, basi ningekua wa mwanzo kumuabudu mtoto huyo mnayedai, Ametakasika Allah Mtukufu na kuwa na mke na mtoto».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net