Az-Zukhruf 43:7
الزخرفوَمَا يَأْتِيهِم مِّن نَّبِىٍّ إِلَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
Na hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli. [7]
[7] Wala hawajii Mtume yeyote kuwakumbusha Haki ila huendelea na kumfanyia maskhara.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawajiwi na Nabii yoyote isipokuwa huwa wakimcheza shere kama vile watu wako walivyokucheza shere, basi tukawaangamiza wale waliowakanusha Mitume wetu, nao walikuwa ni wenye nguvu kali na ushujaa wa kivita kuliko watu wako, (ewe Mtume).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net