Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 8

Az-Zukhruf 43:8

الزخرف

فَأَهْلَكْنَآ أَشَدَّ مِنْهُم بَطْشًا وَمَضَىٰ مَثَلُ ٱلْأَوَّلِينَ

Maana

Na tuliwaangamiza waliokuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tuliwaangamiza walio kuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita. [8]

[8] Basi tuliwateketeza walio kadhibisha walio tangulia; na hao walikuwa wamewazidi makafiri wa Makka kwa nguvu na ushupavu. Basi wasidanganyike hawa na ujabari wao. Na zilikwisha tangulia katika Qur'ani hadithi za ajabu za watu wa kale, za kuwafanya wenginewe wazingatie. Basi enyi mnao kanusha! Zingatieni!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yashapita mateso ya wa mwanzo kwa kuangamizwa kwa sababu ya ukanushaji wao, ujeuri wao na kuwacheza shere Mitume wao. Katika haya pana maliwazo kwa Nabii, (rehema na amani zimshukie).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net