Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 67

Az-Zukhruf 43:67

الزخرف

ٱلْأَخِلَّآءُ يَوْمَئِذٍۭ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا ٱلْمُتَّقِينَ

Maana

Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui wao kwa wao, isipokuwa wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao, isipo kuwa wachamngu. [67]

[67] Marafiki walio kusanyika duniani kwa upotovu, watakuwa maadui wao kwa wao siku itakapo wafikia Saa kwa ghafla, na yatakatika mapenzi yote, ila mapenzi ya wenye kuogopa, nao wangali duniani, kuiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wakashikamana huko duniani katika kumt'ii Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Marafiki katika kumuasi Allah Mtukufu duniani watatengana wao kwa wao Siku ya Kiyama. Lakini wale waliofanya urafiki juu ya uchaji Allah Mtukufu, urafiki wao utadumu duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net