Az-Zukhruf 43:68
الزخرفيَـٰعِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ ٱلْيَوْمَ وَلَآ أَنتُمْ تَحْزَنُونَ
Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika. [68]
[68] Mwenyezi Mungu atawaambia wachamngu kwa kuwafanyia hishima: Enyi waja wangu! Leo msikhofu adhabu yoyote, wala msihuzunike. Mmekwisha salimika na adhabu. Na Mwenyezi Mungu amekudhaminieni thawabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wataambiwa hawa wachamungu, «Enyi waja wangu! Hamna khofu yoyote Leo ya kupata mateso yangu, wala nyinyi hamtahuzunika juu ya hadhi za kilimwengu mlizozikosa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net