Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 66

Az-Zukhruf 43:66

الزخرف

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا ٱلسَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

Maana

Je, nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui? [66]

[66] Makafiri hawangojei kitu baada ya kuipuuza Imani ila kuwafikia Saa kwa ghafla, nao wameghafilika nayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakuna chochote wanachokingojea watu wa makundi hayo waliotafautiana kuhusu ‘Ǐsâ isipokuwa ni kujiwa na Kiyama kwa ghafla, na hali wao hawahisi wala hawatambui.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net