Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 65

Az-Zukhruf 43:65

الزخرف

فَٱخْتَلَفَ ٱلْأَحْزَابُ مِنۢ بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ

Maana

Lakini makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao waliodhulumu kwa adhabu ya siku chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao walio dhulumu kwa adhabu ya siku chungu. [65]

[65] Makundi mbali mbali yakakhitalifiana baina ya Wakristo baada ya Isa, kwa kufarikiana juu yake. Maangamizo yatawafika hao walio dhulumu kwa waliyo yasema juu ya Isa ya ukafiri, watapata adhabu kali na chungu Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo makundi ya watu yakatafautiana kuhusu jambo la ‘Ǐsâ, amani imshukie, na wakawa mapote: kati yao kuna waliokubali kuwa yeye ni mja wa Allah Mtukufu na ni Mtume Wake, na hiyo ndio kauli ya kweli, na kati yao kuna wanaodai kuwa yeye ni mwana wa Allah Mtukufu, na kati yao kuna wanaosema kwamba yeye ni Allah Mtukufu, Ametukuka Allah Mtukufu kutukuka kukubwa na kutakasika na neno lao hilo. Basi maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama ni yenye kuwapata wale waliomsifu ‘Ǐsâ kwa sifa ambazo sizo zile Allah Mtukufu Alizomsifu nazo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net