Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 64

Az-Zukhruf 43:64

الزخرف

إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ رَبِّى وَرَبُّكُمْ فَٱعْبُدُوهُ ۚ هَـٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ

Maana

Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyonyooka.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi Muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. [64]

[64] Hakika Mwenyezi Mungu, peke yake, ndiye Muumba wangu, na ni Muumba wenu, basi muabuduni Yeye pasi mwenginewe. Na ihafidhini sharia yake. Hii ninayo kuitieni muifuate ni Njia Iliyo Nyooka itakayo kufikisheni kwenye uwokovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Mola wangu na Mola wenu nyote, basi muabuduni Yeye Peke Yake na msimshirikishe na Yeye kitu chochote. Hili nililowaamrisha la kumcha Allah Mtukufu na kumpwekesha kwa ustahiki wa kuabudiwa ndio njia iliyonyooka, nayo ni Dini ya Allah Mtukufu ya kweli Ambaye Hakubali kutoka kwa yoyote dini isiyokuwa hiyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net