Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 63

Az-Zukhruf 43:63

الزخرف

وَلَمَّا جَآءَ عِيسَىٰ بِٱلْبَيِّنَـٰتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُم بِٱلْحِكْمَةِ وَلِأُبَيِّنَ لَكُم بَعْضَ ٱلَّذِى تَخْتَلِفُونَ فِيهِ ۖ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Maana

Na alipokuja Isa na ushahidi ulio wazi, alisema: 'Nimewajia na hekima na ili niwaeleze baadhi ya yale mliyokhitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnitii mimi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na alipo kuja Isa na dalili zilizo wazi, alisema: Nimekujieni na hikima, na ili nikuelezeni baadhi ya yale mliyo khitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnit'ii mimi. [63]

[63] Na alipo tumwa Isa kwa Wana wa Israili naye ana miujiza iliyo wazi, na Ishara zenye kubainisha, aliwaambia: Nimekujieni na sharia yenye hikima nzuri, inayo kuiteni muifuate Tawhidi (Imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja). Na nimekujieni nikubainishieni baadhi ya mambo mnayo khitalifiana kwayo katika mambo ya Dini ili mpatane kwenye Haki. Basi iogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu, na mnit'ii mimi katika hayo ninayo kuitieni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ‘Ǐsâ alipowajia Wana wa Isrãîl kwa dalili zilizo wazi alisema, «Nimewajia na unabii, na ili niwaeleze baadhi ya mambo ya yale mnayotafautiana kwayo katika mambo ya Dini. Basi mcheni Allah Mtukufu kwa kufuata amri Zake na kuepuka makatazo Yake, na mnitii mimi katika yale ninayowaamrisha ya kumcha Allah Mtukufu na kumtii».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net