Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 31

Az-Zukhruf 43:31

الزخرف

وَقَالُوا۟ لَوْلَا نُزِّلَ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنَ ٱلْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ

Maana

Na walisema: 'Kwa nini Qur-ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walisema: Kwa nini Qur'ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii? [31]

[31] Na washirikina, kwa kumdharau Muhammad na kuona haiwezi kuwa yeye ateremshiwe Qur'ani, walisema: Kwa nini basi hii Qur'ani, ambayo yeye anadai kuwa ni Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, asiteremshiwe mtu mkubwa mtukufu katika watu wa Makka au T'aif?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa washirikina wa kikureishi walisema, Iwapo hii Qur’ani inatoka kwa Allah Mtukufu kikweli, basi si ateremshiwe mtu mkubwa (mwenye cheo) kutoka miji hii miwili: (Makkah au Ţāif.)

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net