Az-Zukhruf 43:32
الزخرفأَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۚ وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَـٰتٍ لِّيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا ۗ وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ
Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wengineo wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya. [32]
[32] Funguo za Utume hazimo katika mikono ya washirikina, hata wao wawakabidhi watu wenye vyeo. Sisi tumewapangia maisha yao kwa kuwa wao wenyewe hawajiwezi. Na tumewafadhilisha baadhi juu ya wengine katika riziki na vyeo, na kwa hivyo baadhi yao huwafanya wengineo wawasaidie na wawatumikie katika kutimiza haja zao, ili wategemeane katika kutafuta maisha na kupanga uhai. Na Unabii na yaliyo khusiana nayo katika neema za Akhera na dunia, ni bora kuliko vyeo vyote vya duniani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, wao ndio wanaougawa huu utume wakauweka wanapotaka? Sisi tumewagawia wao maisha yao katika uhai wao wa kilimwengu ya riziki na vyakula, na tumewainua daraja baadhi yao juu ya wengine : huyu ni tajiri na huyu ni masikini, huyu ana nguvu na huyu ni mnyonge, ili baadhi yao wawe ni wenye kutumiwa na wengine katika maisha. Na rehema ya Mola wako, (ewe Mtume), ya kuwatia wao Peponi ni bora kuliko takataka za dunia zenye kutoweka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net