Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 30

Az-Zukhruf 43:30

الزخرف

وَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلْحَقُّ قَالُوا۟ هَـٰذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِۦ كَـٰفِرُونَ

Maana

Na ilipowafikia Haki wakasema: 'Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ilipo wafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa. [30]

[30] Na ilipo teremka Qur'ani kuwaongoza kwenye Tawhid wakaongeza juu ya ushirikina wao kuita Qur'ani : "uchawi" na "kiini macho", kwa kejeli. Na wakashikilia ukafiri wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ilipowajia Qur’ani kutoka kwa Allah Mtukufu walisema, «Hii uliyotuletea ni uchawi wa kuturogea nao, na si wahyi unaotoka kwa Allah Mtukufu, na sisi tunaukanusha».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net