Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 29

Az-Zukhruf 43:29

الزخرف

بَلْ مَتَّعْتُ هَـٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمْ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلْحَقُّ وَرَسُولٌ مُّبِينٌ

Maana

Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume aliyebainisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume aliye bainisha. [29]

[29] Washirikina hawakutimiza matumaini ya Ibrahim, wala Mimi sikuwapatiliza papo kwa papo, bali nimewastarehesha hawa ulio nao, ewe Muhammad, na niliwastarehesha baba zao kabla yao kwa namna mbali mbali za neema, mpaka ilipo teremka Qur'ani kuwaitia Haki, na akawajia Mtume mwenye kubaini wazi akiwaita.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Bali niliwastarehesha hawa washirikina wa watu wako, ewe mtume, na wazazi wao kabla yao kwa uhai, sikuwaharakishia adhabu kwa ukanushaji wao mpaka ikawajia Qur’ani na Mtume wa kuwabainishia wanachokihitajia katika mambo ya Dini yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net