Az-Zukhruf 43:28
الزخرفوَجَعَلَهَا كَلِمَةًۢ بَاقِيَةً فِى عَقِبِهِۦ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee. [28]
[28] Kwa kuwatangazia hivyo, likawa hilo Neno la Tawhidi, ni neno lenye kubakia katika dhuriya zake, ili wapate kulirejelea, waliamini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Ibrāhĩm, amani imshukie, alilifanya neno la kumpwekesha Allah Mtukufu (Lā ilāha illā Allāh) ni lenye kusalia baada yake, kwa kutarajiwa warudi kumtii Mola wao na kumpwekesha. Na kutubia kutokana na ukanushaji wao na dhambi zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net