Az-Zukhruf 43:26
الزخرفوَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦٓ إِنَّنِى بَرَآءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ
Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake na kaumu yake: 'Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyaabudu.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu, [26]
[26] Na ewe Muhammad! Waambie hao wanao kanusha hadithi ya Ibrahim pale alipo mwambia baba yake: Hakika mimi nimejitenga mbali na ibada ya kuiabudu hii miungu yenu ya uwongo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kumbuka, ewe Mtume, pindi aliposema Ibrāhĩm alipomwambia baba yake na watu wake waliokuwa wakiabudu vitu ambavyo watu wako, ewe mtume, wanaviabudu, ”Hakika mimi najitakasa na vile mnavyoviabudu badala ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net